1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Upinzani Bangladesh waitisha mgomo wa nchi nzima Jumapili

28 Oktoba 2023

Chama kikuu cha upinzani nchini Bangladesh kimeitisha mgomo wa nchi nzima kesho Jumapili baada maandamano iliyoyaitisha leo kumtaka waziri mkuu wa nchhi hiyo kujiuzulu kusambaratika.

Polisi wakiwatawanya waandamanaji Bangladesh
Polisi wakiwatawanya waandamanaji BangladeshPicha: Munir Uz Zaman/AFP/Getty Images

Maandamano ya leo yalisambaratika kufuatia makabaliano makali baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama. Polisi mmoja amekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapambano yaliyotokea kati

kati mwa mji mkuu wa nchi hiyo Dhaka pale wafuasi wa upinzani walipoitikia wito wa kuandamana kumshinikiza Waziri Mkuu Sheikh Hasina kuachia madaraka kuelekea uchaguzi unaokuja.

Soma zaidi: Maelfu waandamana Bangladesh kumtaka Waziri Mkuu kujiuzulu

Katibu Mkuu wa chama cha Bangladesh Nationalist  (BNP), ametoa mwito wa mgomo wa nchi nzima kesho ikiwa ni mwendelezo la shinikizo kwa Bibi Hasina aridhie kujiuzulu kupisha maandalizi ya uchaguzi.

Upinzani unataka kuundwe serikali ya mpito isiyoegemea upande wowote wa vyama itakayokuwa na dhima ya kusimamia uchaguzi unaokuja wa mnamo mwezi Januari ili kuufanya uwe huru na wa haki.