1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVisiwa vya Comoros

Upinzani Comoro wawasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo

20 Januari 2024

Wagombea watatu wa upinzani visiwani Comoro wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais Azali Assoumani.

Rais wa Comoro Azali Assoumani | Uchaguzi wa Comoro
Rais wa Comoro Azali Assoumani Picha: REUTERS

Abdallah Mohamad Daoudou, aliyekuwa mgombea wa chama cha upinzani cha Chungwa, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, wanaitaka mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Januari 14.

Upinzani unadai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na visa vya udanganyifu ikiwemo masunduku ya kura kujazwa mapema na zoezi la kupiga kura kukamilika kabla ya muda rasmi wa kufunga vituo vya kura.

Serikali hata hivyo imekanusha madai hayo.

Rais Azali Assoumani aliyekuwa akishindana na wapinzani watano, alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 62.97 ya kura. Upinzani umepinga matokeo hayo na kuandaa maandamano ambayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja na kuacha watu wengine 25 na majeraha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW