Upinzani DRC waanzisha kampeni ya "Kwaheri Kabila"
23 Novemba 2016Matangazo
Kampeni hiyo iliyopewa jina la "Kwaheri Kabila" inamtaka rais huyo anayeshutumiwa kwa kuchelewesha chaguzi, kuondoka madarakani bila ya masharti yoyote na kutangaza waziwazi kuwa hatong'angania madaraka.
Mmoja wa waandaaji wa kampeni hiyo, Merveille Gozo, aliwaambia waandishi wa habari hapo jana (Novemba 22) kuwa wamekusanyika kuwaarifu watu wa Congo na jumuiya ya kimataifa kuhusu kampeni hiyo.
Gozo amesema wanapanga kufanya maandamano ya amani kuanzia Ijumaa kuashiria ni muda kwa Kabila kuingia katika kumbukumbu za historia kwa kukabidhi madaraka.
Katiba ya Congo inamzuia Rais Kabila kugombea muhula mwingine, lakini muafaka wa kisiasa na baadhi ya vyama vya upinzani umempa nafasi ya kuhudumu hadi mwaka 2018 baada ya kuitisha uchaguzi.