1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani DRC waitisha maandamano kupinga mageuzi ya katiba

21 Novemba 2024

Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewataka wananchi kuandamana kupinga mpango wa Rais Felix Tshisekedi kuandika katiba mpya.

Rais Felix Tshisekedi
Rais Felix Tshisekedi Picha: Arsene Mpiana/AFP

Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewataka wananchi kuandamana kupinga mpango wa Rais Felix Tshisekedi kuandika katiba mpya.

Tshisekedi alitangaza mwezi uliyopita kuundwa kwa tume ya kuandaa katiba mpya, hatua ambayo imeibua hofu miongoni mwa wapinzani kuhusu uwezekano wa kubadilishwa kwa ukomo wa mihula ya urais.

Wanasiasa wa upinzani, akiwemo Rais wa zamani Joseph Kabila na waliokuwa wagombea urais Martin Fayulu na Moise Katumbi, wamepinga mpango huo, wakisema katiba iliyopo inalenga kuzuia mwelekeo wa kiimla na kuhakikisha mabadiliko ya kidemokrasia ya uongozi.

Tshisekedi, ambaye alichaguliwa tena Desemba mwaka jana katika uchaguzi uliopingwa na upinzani, amekuwa akikosolewa kwa juhudi zake za kubadilisha katiba ya mwaka 2006, akidai kuwa ni ya kizamani.

Wapinzani wana wasiwasi kuwa anaweza kujaribu kuongeza ukomo wa mihula miwili ya miaka mitano ili aendelee kubaki madarakani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW