1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Upinzani wamshutumu Netanyahu kumfuta kazi Gallant

6 Novemba 2024

Viongozi wa upinzani wa makundi mbalimbali ya kisiasa nchini Israel wamemkosoa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kumwachisha kazi waziri wake wa ulinzi. Wanasema hatua hiyo inatishia usalama wa taifa.

Israel | Benjamin Netanjahu na Yoav Gallant
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanjahu akizungumza na aliekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.Picha: DEBBIE HILL/POOL/AFP via Getty Images

Katiku kikao cha pamoja cha waandishi habari, wapinzani wamemtuhumu Netanyahu kwa kuyatanguliza mbele maslahi yake ya kisiasa badala ya nchi.

Netanyahu alimtimua Yoav Gallant baada ya tofauti zao za wazi kuhusu operesheni ya kijeshi ya Israel ya kulipiza shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel Oktoba 6 mwaka jana.

Soma pia:Netanyahu amfuta kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant

Kiongozi mkuu wa upinzani Benny Gantz, ambaye alijiondoa katika serikali ya Netanyahu mwezi Juni kwa kukosa mpango wa baada ya vita vya Gaza, amesema hatua hiyo ya Netanyahu imekuja wakati mbaya akiongeza kuwa ni "uzembe mkubwa wa kiusalama."

Uamuazi wa kumfuta kazi Gallant imejiri wakati ambao Israel inapambana kuongeza idadi ya askari, huku vikosi vya ardhini vikitumwa kukabiliana na Hamas huko Ukanda wa Gaza na Hezbollah nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW