1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Kenya wapeleka kesi yao The Hague

22 Januari 2008

NAIROBI:

Mgogoro wa kisiasa wa Kenya sasa umeplekwa katika mahakama ya kimataifa.taarifa kutoka Nairobi zinasema kuwa pande zote husika katika mgogoro huo zinaulaumu upande mwingine kwa makosa ya kijinai yaliyofanyika wakati wa ghasia zilizofuata uchaguzi wa uraia wa mwezi jana.Ghasia hizo zilipelekea watu mamia kadhaa kuaawa.

Chana cha upinzani cha Orange Democratic Movement –ODM kimesema kuwa kimetuma malalamiko yake mjini Hague Uholanzi ambako ndio makao makuu ya mahakama hiyo.Chama cha upinzani kinadai kuwa wakuu wa Kenya walitenda maovu dhidi ya binadamu wakati polisi ilipowapiga risasi raia ambao hawakuwa na silaha: hata hivyo serikali inakanusha madai hayo.Serikali kwa upande wake inawalaumu baadhi ya vingozi wa chama cha ODM kwa kuwachochea wafuasi wao kutenda makosa ya kijinai baada ya rais Mwai kibaki kutangazwa kama mshindi wa uchaguzi unaotatanisha wa Disemba 27 ambao ulizusha ghasia karibu nchini kote.

Mahakama ya kimataifa kila mwaka hupokea malaamiko mamia kadhaa lakini mengi hukataliwa.Na mjini Nairobi,vikosi vya usalama vinajaribu kurejesha utulivu kabla ya kuwasili kwa katibu mkuu wa zamani wa Umoja waMataifa – Koffi Annan anaetarajiwa kuwasili leo.Bw Annan na ujumbe wa wapatanishi wengine kutoka afrika wanatarajiwa kukutana na pande mbili za rais Mwai Kibaki na wa upinzani wa Raila Odinga kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa ambao ulianza baada ya Odinga kudai kuwa kulifanyika mizengwe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW