Upinzani Kongo wadai kuchezewa ´rafu` kuelekea uchaguzi
15 Desemba 2023Matangazo
Upinzani umeeleza wasiwasi wao kuhusu wagombea kuzuiwa kufanya kampeni, uchelewashaji wa orodha kamili ya wapiga kura na kadi za kura zisizosomeka.
Mvutano umeongezeka kuelekea wiki za mwisho za kampeni kabla ya uchaguzi wa Disemba 20. Rais Felix Tshisekedi amelalamikia kile alichokiita "uwanja usiokuwa sawa" na kuzituhumu mamlaka kwa kupanga njama ya kuchakachua matokeo.
Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi ya Kongo, CENI, imekanusha madai hayo.
CENI pia imepinga ukosoaji dhidi yake kwa kushindwa kuandaa uchaguzi ulio huru na wa haki kama ilivyoahidi, licha ya changamoto ya usafirishaji wa vifaa vya kura hiyo katika taifa hilo la pili kwa ukubwa barani Afrika.