Upinzani Kongo wauonya utawala kuhusu mageuzi ya katiba
26 Oktoba 2024Martin Fayulu, ambaye alikuwa kwenye nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwaka jana, amesema Katiba ya sasa haimzuii mtu yeyote kufanya kazi. Kiongozi huyo wa upinzani ametoa wito kwa raia wa Kongo kuwa tayari kuzuia jaribio lolote la magaeuzi ya katiba.
Akiwa ziarani mjini Kisangani, Kaskazini-Mashariki mwa Kongo, Rais Felix Tshisekedi aliahidi kuteua mwakani, tume ya kitaifa kwa jali ya kuandaa katiba mpya. Tshisekedi amesema katika ya hihi sasa inapitwa na wakati.
Hatua hiyo imeibua wasiwasi miongoni mwa wapinzani, wakimshutumu kutaka kubakia madarakani. Katiba ya sasa ya Kongo ni ya sita tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni Ubelgiji mnamo 1960.
Mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa shirika la The Struggle for Change (LUCHA) linalotetea haki za kijamii Fred Bauma amesema Tshisekedi anaendelea kukaidi katiba wakati aliapa kuilinda na kuitetea wakati alipoapishwa mapema mwaka huu.