1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani nchini DRC wapinga daftari la wapiga kura

Saleh Mwanamilongo12 Aprili 2018

Vyama vikuu vya upinzani kikiwemo kile cha UDPS vimepinga daftari la wapiga kura liliotangazwa na tume huru ya uchaguzi na kuomba kuwapo na ukaguzi wa kimatifa wa daftari hilo.

28412987-Kopie.
Picha: picture alliance/dpa

Vyama vikuu vya upinzani kikiwemo kile cha UDPS vimepinga daftari la wapiga kura liliotangazwa na tume huru ya uchaguzi na kuomba kuwapo na ukaguzi wa kimatifa wa daftari hilo. Pia umepinga matumizi ya mfumo wa uchaguzi wa kielektroniki ambao tume ya uchaguzi tayari imeuagiza kutoka Korea ya kusini. Upinzani umesema kwamba mfumo huo unalenga kuiba kura kwa faida ya chama tawala.

Kwenye taarifa yao ya pamoja Felix Tshisekedi kiongozi wa chama cha UDPS, Vital Kamerhe wa chama cha UNC,Pierre Lumbi anayewakilisha vyama vya ENSEMBle vinavyomuunga mkono Moise Katumbi, na Eve Bazaiba katibu mkuu wa chama cha MLC cha Jeanpierre Bemba waelezea wasiwsai wao kuhusu daftari la wapigaji kura ambalo wamesema limejaa kasoro. Kwa hiyo viongozi hao wa upinzani wameomba kuwepo na ukaguzi wa daftari zote za wapiga kura, Eve Bazaiba ni msemaji wao.

Upinzani unadai mfumo wa kielektroniki katika uchaguzi ni njama ya kuiba kura.Picha: Getty Images/AFP/F. Scoppa

"Tume huru ya uchaguzi imetangaza idadi ya wapigaji kura milioni 40 ambayo siyo ya kweli na iliyo jaa kasoro chungu nzima. Tulisubiri kuona zaidi ya wapigaji kura kwenye daftari hizo. Tumeshuhudia pia idadi kubwa ya watu waliofutwa kwenye dafatari hizo kwamba walijiandfikisha zaidi ya mara moja ,wengine wakiwa ni watoto wa chini ya umri wa miaka 18,hiyo inaonyesha wazi jaribio la udanganyifu. Tunataka kuona ukaguzi wa kimataifa ukifanyika kwa haraka".

Viongozi hao wa upinzani nchini Kongo wamepinga mfumo wa uchaguzi wa kutumia mashine ya kupigia kura, wakielezea kwamba ni njama ya kuiba kura.

Wiki iliopita tume ya uchaguzi ilitangaza daftari za wapigaji kura katika kila jimbo la uchaguzi, mwenye kiti wa tume ya uchaguzi Corneille Nangaa alisema kwamba baada ya kufanya ukaguzi tume huru ilifuta majina ya watu milioni 6.3 kwa sababu milioni 5 walikuwa ni watu waliojiandikisha zaidi ya mara mmoja na wengine laki tisa ni watoto wa chini ya umri wa miaka 18. Tume ya uchaguzi imesema imewasilisha dafatari hizo kwenye vyombo vya kishera kwa sababu ni ukiukaji wa sheria ya Kongo na kanuni za uchaguzi.

Chama tawala kimeunga mkono, utaratibu wa tume ya uchaguzi wa kukagua daftari za wapiga kura. John Omombo ni katibu mkuu wa chama cha MRL, kinachomuunga mkono rais Joseph kabila.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph KabilaPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

"Katiba yetu kwenye kipengee cha 211 imeipa tume huru ya uchaguzi mamlaka ya kuchangia ilikuboresha taratibu za uchaguzi na kura ya maoni. Kwa hiyo kwetu sisi tunapongeza hatua yeyote ile itakayo chukuliwa na tume ya uchaguzi iliuchaguzi huo ufanyike katika mazingitra bora".

Tume huru ya uchaguzi inaelezea kwamba matumizi ya kumpyuta ni kwa ajili ya kupunga garama za uchaguzi. Marekani na Korea ya kusini pia zilielezea wasiwasi wao kuhusu matumizi ya kompyuta wakati wa u haguzi, zikielezea kwamba Kongo bado haija kuwa na miundo mbinu bora kwa matumizi ya mfumo huo wa uchaguzi.

Daftari la uchaguzi ni muhimu kwa ajili ya kuwepo na sheria ya ugawanyaji viti bungeni. Kulingana na kalenda ya uchaguzi,sheria hiyo inatakiwa kusomwa bungeni na kuidhinishwa na rais Kabila kabla ya mei 8.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW