1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani nchini Mauritius washinda uchaguzi kwa kishindo

12 Novemba 2024

Muungano wa upinzani nchini Mauritius umeshinda uchaguzi wa nchi hiyo kwa kishindo, ukidhibiti viti vyote bungeni katika moja ya anguko kubwa la serikali iliyoko madarakani.

Mauritius
Upinzani nchini Mauritius washinda uchaguzi kwa kishindoPicha: AFP

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa katika majimbo kadha kote nchini humo, muungano tawala unaoongozwa na Waziri Mkuu Pravind Jugnauth, umeshindwa kupata viti vyoyote kati ya 62 vinavyoamuliwa moja kwa moja na wapiga kura.

Jugnauth alitangaza kushindwa hata kabla ya matokeo yote kutolewa, akisema kwamba muungano wake wa Vuguvugu la Wanamgambo wa Kisosholisti unaelekea kushindwa vibaya, huku upinzani ukionekana kudhibiti majimbo yote 21 ya nchi.

Raia wa Mauritius wanapiga kura kuwachagua wabunge

Ushindi wa muungano wa upinzani wa Alliance for Change, unamrejesha mamlakani Navin Ramgoolam kuwa waziri mkuu mpya.

Mwanasiasa huyo aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu kutoka mwaka 1995 hadi 2000 na kwa mara nyingine kati ya 2005-2014.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW