1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Upinzani Poland watazamiwa kupata wabunge wengi

17 Oktoba 2023

Vyama vya upinzani nchini Poland vinavyounga mkono Umoja wa Ulaya vinatazamiwa kushinda viti vingi vya bunge.

Huenda matokeo ya uchaguzi Poland yakamaliza miaka minane ya utawala wa chama cha kizalendo cha Sheria na Haki.
Huenda matokeo ya uchaguzi Poland yakamaliza miaka minane ya utawala wa chama cha kizalendo cha Sheria na Haki.Picha: REUTERS

Vyama hivyo vitatu vya upinzani kwa pamoja vina asilimia 53 huku chama tawala PiS kikiwa na asilimia 35.6 baada ya asilimia 99 ya kura zote kuhesabiwa.

Mkuu wa zamani wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk anayeuongoza upinzani aliutaja uchaguzi huo wa ubunge uliofanyika Jumapili kuwa "nafasi ya mwisho” ya kuokoa demokrasia.

Uchaguzi huo, ulishuhudia idadi kubwa zaidi ya watu waliojitokeza kupiga kura tangu kuanguka kwa Ukomunisti.

Huenda matokeo hayo yakamaliza miaka minane ya utawala wa chama cha kizalendo cha Sheria na Haki.