Upinzani Rwanda wataka msaada kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya
7 Juni 2010Vyama vitatu vya upinzani nchini Rwanda vimeiomba Marekani, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuingilia kati na kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kufungua milango ya ushindani wa kisiasa kuviwezesha vyama hivyo kushiriki katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika tarehe 9 mwezi Agosti mwaka huu.
Katika barua iliyotumwa kwa pande hizo tatu, vyama hivyo, Democratic Green Party, PS Imberakuri na FDU Inkingi, vimeeleza kuwa licha ya juhudi zote za kisheria kutaka kushiriki katika uchaguzi huo, hadi sasa serikali imeviwekea aidha kwa kuvinyima usajili, ama kuweka vizingiti vingine vinavyokwamisha shughuli zao. Mwandishi wetu wa mjini Kigali, Daniel Gakuba ametutumia ripoti ifuatayo.
Mwandishi, Daniel Gakuba
Mpitiaji, Peter Moss
Mhariri, Josephat Charo