1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Tanzania unataka uchaguzi urudiwe tena

Yusra Buwayhid
31 Oktoba 2020

Vyama vikuu viwili vya upinzani nchini Tanzania vinataka uchaguzi urudiwe tena, na wanawahimiza wananchi kumiminika barabarani kwa "Maandamano ya amani" kuanzia Jumatatu.

Tansania Wahlen
Picha: Reuters

Vyama hivyo vinadai kuwa uchaguzi uliofanyika Oktoba 28 ulijawa na visa vya udanganyifu. Hayo yanajiri muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza Rais John Magufuli kuwa ni mshidi wa uchaguzi huo kwa asilimia 84.

Vyama vya ACT Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA vimepinga matokeo ya uchaguzi katika ngazi za udiwani, ubunge, uwakilishi na urais.

Soma zaidi: Tume ya Uchaguzi Tanzania: Magufuli ndiye mshindi wa urais

"Kilichotokea Oktoba 28 haukuwa uchaguzi bali ni kuivuruga demokrasia,” Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliwaambia waandishi wa habari, akisisitiza kwamba zaidi ya watu 20 waliuawa wakati wa upigaji kura. Aliongeza: "Tunatangaza mandamano ya amani yasiyo na mwisho kuanzia Jumatatu hadi mahitaji yetu yatekelezwe. "

Kati ya jumla ya viti 256 bungeni ACT Wazalendo imeshinda viti vinne, CUF viti vitatu na CHADEMA kiti kimoja. Tume ya uchaguzi ilimtangaza John Magufuli usiku wa jana kuwa ameshinda kwa asilimia 84 huku mpinzani wake Tundu Lissu akipata asilimia 13.04 pekee.

Maalim Seif Shariff Hamad akiwa Freeman MbowePicha: DW/S. Khamis

Polisi: Hakuna mauaji yaliyotokea

Mbali na madai ya upinzani ya ukiukaji mkubwa kabla na wakati wa kupiga kura, waangalizi wengine wanasema taifa hilo la Afrika Mashariki halikuzingatia ipasavyo maadili ya kidemokrasia na badala yake limechukuwa mwelekeo tofauti na ule uliofuatwa miaka mitano iliyopita.

Madai yanayotajwa ni pamoja na kukataliwa kwa maelfu ya waangalizi wa uchaguzi, kuzimwa kwa mtandao wa intaneti na kujazwa kwa kura za bandia kwenye visanduku vya kupigia kura.

Tundu Lissu ayapinga matokeo

02:36

This browser does not support the video element.

Katika tangazo lake la mwisho Ijumaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kimesema uchaguzi ulikuwa wa halali.

Soma zaidi: Maoni: Mbali na dosari zilizojitokeza Tanzania, amani na umoja vitawale

Asilimia 50 ya wapiga walijitokeza kupiga kura, katika uchaguzi huo.

Polisi wamekiri kukamatwa kwa watu wengi karibu na uchaguzi lakini hakuna mauaji yaliyotokea.

Vyanzo: (rtre,ap)

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW