1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Ujerumani wataka wahamiaji haramu wadhibitiwe

23 Januari 2025

Kiongozi wa chama mbadala wa Ujerumani cha AfD Alice Wiedel ametaka kura ya haraka ya bunge kuhusu kufunga mipaka ya nchi baada ya shambulizi kwenye mji wa Aschaffenburg, kusini mwa Ujerumani.

Alice Weidel kiongozi wa AfD anayegombea ukansela wa Ujerumani
Chama cha AfD chenye siasa kali za mrengo wa kulia Ujerumani washinikiza hatua za kukabiliana na wahamiaji haramuPicha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

Weidel, mgombea wa ukansela kupitia AfD, katika uchaguzi wa Februari 23, amesema ni lazima kambi ya kihafidhina ya CDU/CSU iachane na msimamo wake wa kutokushirikiana na chama hicho cha msimamo mkali wa kulia ili kupitisha sheria inayohusiana na "kufungwa kwa mipaka na kuwarejesha wahamiaji haramu.

Waziri Mkuu wa Jimbo la Bavaria Markus Söder naye pia ametaka kufungwa kwa mipaka katika kukabiliana na wahamiaji haramu kufuatia shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu wawili.

Kiongozi huyo wa Chama cha kihafidhina cha Christian Social Union (CSU) katika jimbo hilo, amesema kauli mbiu yao ni lazima iwe usalama kwanza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW