1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani utakata rufaa kupinga urais wa Tinubu Nigeria

7 Septemba 2023

Wagombea wakuu wa upinzani katika nafasi ya urais wa Nigeria kupitia wanasheria wao wamesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama uliothibitisha ushindi wa rais Bola Tinubu.

Nigeria | Bola Tinubu
Picha: Sunday Aghaeze/Nigeria State House via AP/picture alliance

Wagombea wakuu wa upinzani katika nafasi ya urais wa Nigeria kupitia wanasheria wao wamesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama uliothibitisha ushindi wa rais Bola Tinubu katika uchaguzi wa urais wa mwezi Februari ambao ulikuwa na utata.

Soma pia: Mahakama Nigeria kuamua kuhusu ushindi wa Tinubu

Wagombea Atiku Abubakar wa chama cha People's Democratic Party na Peter Obi wa Labour Party's ambao walishika nafasi ya pili na yatatu kwenye uchaguzi huo, waliwasilisha mahakamani kesi ya kutaka uchaguzi ufutwe kwa madai ya wizi wa kura na mawakala kushindwa kuchapisha matokeo ya uchaguzi kupitia mtandao.

Soma pia: Rais wa Nigeria akabidhiwa mikoba ya ECOWAS

Lakini Mahakama ya rufaa ya Nigeria hapo jana ilitupilia mbali maombi yao katika hukumu ambayo iliyosomwa kwa zaidi ya saa 11.

Wakili wa Obi, Livy Uzoukwu, aliwaambia wanahabari kuwa timu yake itaipitia hukumu kikamilifu na kukata rufaa katika Mahakama ya Juu.

Soma: Bola Tinubu aapishwa kuwa Rais wa Nigeria

Rufaa katika Mahakama ya Juu nchini humo, inapaswa kuwasilishwa ndani ya 14 siku kutoka tarehe ya uamuzi wa mahakama na Mahakama Kuu ina siku 60 za kusikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi wake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW