Upinzani wa Haiti wapinga mpango wa kimataifa wa amani.
22 Februari 2004Matangazo
PORT-AU-PRINCE: Nchini Haiti Rais anayebishwa Jean Bertrand Aristide ameukubali ule mpango wa amani wa kimataifa, unaoshauri kuwa upinzani ushirikishwe serikalini. Mwungano wa Upinzani Democratic Plattform, unaosisitiza kuwa Rais Aristide ajiuzulu, umeukataa mpango huo. Baada ya kufanyika mazungumzo pamoja na ujumbe wa kimataifa chini ya uongozi wa Marekani, upinzani huo umeomba upewe muda mpaka Jumatatu kuamua iwapo uukubali mpango huo. Wanamgambo wa kiasi wanaopigana vita vya kumwangusha Rais Aristide wanadhibiti majimbo kadha huko Haiti ya Kaskazini. Hapo jana waliuawa watu wawili na wengine 20 walijeruhiwa mapigano yalipopamba moto katika mji mkuu Port-Au-Prince, kiliarifu Chama cha Msalaba Mwekundu.