1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wa Venezuela wazidisha mbinyo wake:

6 Machi 2004

CARACAS: Nchini Venezuela upinzani umetangaza kuwa umeandaa maandamano makubwa hii leo dhidi ya Rais Hugo Chavez. Wakati huo huo upinzani huo unafanya mapatano pamoja na tume ya uchaguzi juu ya mwito wao uliokataliwa kuwa Rais Chavez aachishwe wadhifa wake. Hapo Jumanne tume ya uchaguzi iliukataa mwito huo kufuatana na hoja kuwa hazijapatikana zile saini miliyoni 2.4 kama vile inavyotakiwa na sheria. Kutoka jumla ya kura miliyoni tatu zilizotolewa ni nusu tu zinazokubalika, ilisema tume hiyo ya uchaguzi. Kwa mara nyingine tena Rais Chavez ameishutumu Marekani kuwa inachochea mgogoro wa siasa za ndani nchini Venezuela.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW