Upinzani waapa kuchafua shughuli ya kuapishwa Maduro
7 Januari 2025Maduro, mwenye umri wa miaka 62, aliyeliongoza taifa hilo lenye utajiri wa mafuta tangu kufariki dunia kwa shujaa wake, Hugo Chavez, anatuhumiwa na upinzani na washirika wao wa Magharibi kwa kung'ang'ania madarakani, kwa msaada wa vyombo vya dola.
Soma zaidi: Marekani yamtambua Gonzalez Urrutia kama rais mteule wa Venezuela
Maduro anatazamiwa kuapishwa siku ya Ijumaa (Januari 10) kwa muhula wake wa tatu wa miaka mingine sita, baada ya kutupilia mbali tuhuma za kuiba kura kwenye uchaguzi wa Julai dhidi ya mgombea wa upinzani, Edmundo Gonzalez Urrutia, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni.
Jana Jumatatu, Gonzalez Urrutia mwenye umri wa miaka 75 alikutana na Rais Joe Biden kwenye Ikulu ya White House, akiwa kwenye kampeni yake ya kuitaka jumuiya ya kimataifa kumshinikiza Maduro kuachia madaraka.