1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Upinzani wakosoa uchaguzi wa rais Tunisia

6 Oktoba 2024

Watunisia wanapiga kura katika uchaguzi wa rais ambao upinzani unasema umeghubikwa na ukosefu wa uaminifu na uadilifu.

Tunisia | Uchaguzi wa rais
Mwanamke akipiga kura katika kituo cha upigaji kura wakati wa uchaguzi wa rais Tunisia.Picha: Zoubeir Souissi/REUTERS

Uchaguzi huo unamkutanisha rais aliye madarakani Kais Saied na wapinzani wawili pekee ambao mmoja wao yuko jela.

Mapema wiki hii, mahakama ya Tunisia ilithibitisha kifungo cha miezi 20 kwa mgombea urais Ayachi Zammel, mfanyabiashara na mwanasiasa huria, kwa tuhuma za kughushi ridhaa ya uchaguzi.

Soma pia: Mgombea urais Tunisia ahukumiwa miaka 12 jela

Vyama vya upinzani na mashirika ya haki za binadamu yanasalia kuwa na mashaka kuhusu haki ya uchaguzi, huku Tume ya uchaguzi hivi majuzi ikikataa kuwaruhusu wagombea wengine watatu wa urais walioruhusiwa na mahakama kujumuishwa kwenye kinyangayiro hicho baada ya kukata rufaa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW