SiasaSudan Kusini
Upinzani wapuuza wito wa mazungumzo ya amani Sudan Kusini
18 Julai 2025
Matangazo
Pal Mai Deng, msemaji wa chama cha upinzani SPLM-IO, amesema Rais Kiir anapaswa kwanza kuwaachilia viongozi wa kisiasa na kijeshi walioko gerezani ili kudhihirisha nia ya kweli kuhusu mazungumzo hayo.
Kauli ya Rais Kiir imejiri katika hotuba yake wakati wa kufungua tena bunge, akisisitiza haja ya umoja na maridhiano ya kitaifa, akisema "milango ya amani bado iko wazi.”
Hali nchini Sudan Kusini inaendelea kuwa ya wasiwasi baada ya Makamu wa Rais Riek Machar— mpinzani wa zamani wa Kiir — kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani kufuatia shambulio dhidi ya vituo vya jeshi mwezi Machi. Wanachama wengi wa chama cha upinzani wamekimbia nchi kwa hofu ya kukamatwa.