1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Upinzani watoka nje wakati waziri mkuu Modi akihutubia bunge

10 Agosti 2023

Serikali ya waziri mkuu wa India, Narendra Modi imeepuka kuondolewa kwa hoja ya bunge ya kutokuwa na imani baada ya hotuba kali ya Modi katika siku ya mwisho ya mjadala wa siku tatu wa kutokuwa na imani naye.

Indien | Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra ModiPicha: Manish Swarup/AP Photo/picture alliance

Hoja hiyo ilishindwa katika kura ya sauti iliyoitishwa na spika wa bunge, muda mfupi baada ya wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama cha Congress, Rahul Gandhi kutoka nje.

Wabunge hao walitoka wakati Modi alipokuwa akihutubia akitetea rekodi yake, kufuatia hoja hiyo iliyotolewa na muungano mkuu mpya wa upinzani unaoongozwa na chama hicho cha Congress.

Wapinzani hao wanamshinikiza Modi kuzungumzia wazi ghasia mbaya kabisa zilizolikumba jimbo la Manipur, kaskazini mashariki mwa India zinazoibua kitisho cha vita vya kiraia.