1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Upinzani Zimbabwe wapoteza wabunge 15

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Wabunge 15 wa upinzani nchini Zimbabwe wamepoteza viti vyao vya ubunge katika hali isiyoeleweka na ya kutatanisha .

Siku ya Jumanne wabunge hao 15 waliwasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi wa spika wa bunge kutangaza viti vyao vya ubunge kuwa wazi.
Siku ya Jumanne wabunge hao 15 waliwasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi wa spika wa bunge kutangaza viti vyao vya ubunge kuwa wazi.Picha: Reuters/A. Ufumeli

Ni baada ya kile wanachosema mtu aliyejifanya kuwa afisa wa chama kuwaondoa, na bunge likamuunga mkono.

Hatua hiyo imefungua mlango kufanyika kwa chaguzi ndogo ambazo huenda zikakipa chama tawala cha ZANU-PF, kilichoshinda uchaguzi uliozozaniwa wa mwezi Agosti, wingi wa theluthi mbili bungeni unaohitajika kuifanyia mageuzi katiba.

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani Zimbabwe, Citizens Coalition for Change, CC, Promise Mkwananzi amesema hawatakubali tabia hiyo ya dharau dhidi ya katiba na demokrasia yao.

Siku ya Jumanne wabunge hao 15 waliwasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi wa spika wa bunge kutangaza viti vyao vya ubunge kuwa wazi.

Hali hii imesababishwa na barua yenye makosa ya kiserufi iliyoandikwa na mwanamume kwa jina Sengezo Tshabangu ambaye anadai kuwa katibu mkuu wa chama cha CCC, inayosema wabune hao 15 hawakuwa tena wanachama wa chama hicho.

Mwenyekiti wa chama cha CCC Nelson Chamisa alimtaka spika wa bunge apuuzilie mbali ujumbe huo kwa sababu Tshabangu hakuwa mwanachama wa chama hicho, chama hakikuwa na katibu mkuu na hakijamfukuza wala kumuondoa mbunge yeyote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW