1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Upungufu wa fedha taslimu waanza kupungua Nigeria

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Mzozo wa uhaba wa fedha taslimu na misururu mirefu mbele ya mashine za kutolea fedha, ATM nchini Nigeria umeanza kupungua.

Öl Globaler Einfluss Geld Finanzen Nigeria Naira
Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Kuanzia Jumatatu wiki hii mistari ya wateja haionekani mbele ya majengo ya benki mjini Lagos na katika miji mingine mkubwa. Chama cha wafanyakazi cha National Labour Congress, NLC kilikuwa kimeitisha mgomo leo Jumatano, lakini kiliuahirisha jana Jumanne kwa muda wa wiki mbili baada ya kuridhika kuwa Wanigeria walikuwa wanweza kupata pesa tasimu kwa viwango vya kuridhisha. Uhaba wa pesa hizo ulianza mwezi Okoba mwaka jana kufuatia uamuzi wa benki kuu ya nchi hiyo kuweka Februari mwaka huu kuwa mwezi wa mwisho kwa matumizi ya noti za 200, 500 na 1,000 za sarafu ya nchi hiyo, naira, ili zipishe noti mpya zilizokuwa zimetolewa.