Uranium yatishia usalama Arusha
9 Novemba 2012Taarifa hizo zimethibitishwa na kamisheni ya nishati ya Atomiki nchini humo yenye makao yake makuu mjini Arusha.Kamisheni hiyo tayari imeuonya umma kwa jumla na hasa wakulima juu ya kutumia vibaya kemikali hiyo hatari.
Kamisheni hiyo imefahamisha kwamba hatua hiyo inahatarisha sio tu maisha ya wakulima bali hata pia umma kwa jumla. Mamilioni ya watu wanaotumia chakula cha mahindi maharagwe na nafaka nyinginezo zilizohifadhiwa kwa njia ya kutumia kemikali hizo wako katika kitisho kikubwa cha kupata maradhi ya saratani na maradhi mengine.
Shirika la Atomiki lazungumzia suala hilo
Mkurugenzi wa shirika hilo la Atomiki Tanzania Prof Iddi Mkilaha akizungumzia suala hilo amesema kuna baadhi ya wafanyibiashara walaghai wanaoagiza Uraninium kutoka nchi kadhaa jirani na kuuza kamekali hiyo kwa wakulima na kuwadanganya kwamba vumbi la madini hayo ndio njia pekee ya kupambana na wadudu wa mimea na matatizo mengine katika mimea kwa jumla. Hata hivyo taarifa hizi zimezusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa watu akizungumza na Dw kwa njia ya simu hivi punde msemaji wa wizara ya maendeleo ya kigeni kuhusu sera ya Ujerumani ambaye pia ameandika barua ya wazi kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi nishati ya Atomiki duniani IAEA,na ambaye amewahi kutembelea maeneo ya miradi ya Uranium Tanzania kuhusu suala hilo,Ute Koczy amesema "Kinachoendelea Tanzania ,wanaohusika na kadhia hii ,chanzo chake na wanaopigia debe kadhia hii hawajawekwa wazi lakini cha muhimu na msingi ni kwamba ipo haja kubwa kwa serikali ya Tanzania na mashirika husika kuulinda umma na kuutahadharisha.''
Bibi Koczy ambaye ni mbunge wa Ujerumani ameandika pia barua ya wazi juu ya suala hilo kwa rais na waziri mkuu wa Tanzania. Kwa upande wake Prof Mkilaha mkurugenzi mkuu wa TAEC amefahamisha kwamba tayari shirika hilo limefanikiwa kuwatambua baadhi ya wafanyibiashara wanaohusika na kadhi hii na limeshirikiana na polisi kuwakamata.Mtaalamu wa Nuklia katika shirika hilo Dr Mwijarubi akitoa ufafanuzi kuhusu madhara ya kemikali hii amesema pindi mtu anapovuta hewa ya vumbi hilo la madini ya Uranium linaingia moja kwa moja kwenye mapafu na kusababisha saratani ya mapafu na viuongo vingine mwilini. Halikadhalika kwa mujibu wa wataalamu nafaka zilizoingia madini hayo huenda zikasababisha madhara makubwa sio tu kwa wakulima wahusika bali pia kwa wale wakulima wanaosagisha kwenye mitambo ambako imetokea nafaka aina hiyo zimesagishwa.
Katika suala hilo Sudi Mnette amezungumza na Julius Nimbu Mkurugenzi wa Mazingira ofisi ya makamu wa rais wa Tanzania. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri :Mohammed AbdulRahman.