1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ureno yataka kurudia kampeni yake ya 2016

11 Juni 2021

Pereira asema Ureno inataka kurudia kampeni yake ya 2016

Frankreich Euro 2016 Finale Portugal ist Europameister
Picha: Reuters/K. Pfaffenbach

Ureno inalenga kurudia kampeni yake ya mwaka 2016, kushinda tena kombe la mataifa ya Ulaya la Euro mwaka 2020. Soma ziadi  Euro 2016 : Ureno mabingwa wa Ulaya

Kiungo wa kati wa timu hiyo Danilo Pereira amesema kikosi cha Ureno kitajiwakilisha kama mabingwa wa Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa habari Pereira amesema wachezaji wa timu hiyo wana fahari kubwa ya kutetea ubingwa kwa namna hiyo lakini anafahamu kuwa kuna washindani wengine na wanaopendwa zaidi.

Danilo Pereira, aliyevalia jezi nambari 13Picha: Getty Images/AFP/M. Riopa

"Tunasimama pamoja kama kikundi na sote tunafikiria jambo moja sawa: kurudia 2016," alisisitiza  Pereira.

Ureno itashuka dimbani siku ya Jumanne (15.06.2021) kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Hungary itakayochezwa huko Budapest.

Wapinzani wengine katika kundi F ni Ujerumani na mabingwa wa dunia Ufaransa. Ujerumani, Ufaransa na Ureno Kundi moja Euro 2020

DPA

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW