1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi bado yapambana na wanajeshi wa Ukraine waliovuka mpaka

8 Agosti 2024

Wanajeshi wa Urusi wanakabiliana na wa Ukraine katika mkoa wa Kursk katika siku ya tatu ya mojawapo ya matukio makubwa kabisa ya uvamizi wa mpakani katika vita vyao.

Athari za vita kati ya Urusi na Ukraine
Athari za vita kati ya Urusi na Ukraine.Picha: Acting Governor of Kursk Region Alexei Smirnov/Telegram/REUTERS

Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Urusi imesema leo kuwa jeshi la Urusi na walinzi wa mpakani wamewazuia askari wa Ukraine kusonga ndani zaidi katika mkoa wa Kursk kusini magharibi mwa Urusi.

Imesema jeshi linavikabili vikosi vya Ukraine vinavyojaribu kusonga mbele katika eneo hilo kutokea mkoa wa Sumy nchini Ukraine.

Taasisi ya Utafiti wa Vita, yenye makao makuu yake mjini Washington, Marekani, imesema kufikia jana, askari wa Ukraine walikuwa wameingia karibu kilomita 10 ndani ya mipaka ya Urusi lakini taarifa hiyo haikuthibitishwa.

Maafisa wa Ukraine hawajazungumzia ukubwa wa operesheni hiyo karibu na mji wa Sudzha. Rais wa Urusi Vladmir Putin aliuelezea uvamizi huo kuwa ni uchochezi wa kiwango kikubwa.