1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi haitokubali tena mabomba yalipuliwe

3 Machi 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema leo kwamba Urusi haitayaruhusu mataifa ya Magharibi kulipua tena mabomba ya gesi.

Gaspipeline in Oud-Beijerland in den Niederlanden
Picha: ANP/IMAGO

Lavrov ameongeza kwamba Moscow haitayategemea tena Mataifa hayo kama mshirika wa nishati.

Moscow inadai kuwa nchi za Magharibi zilihusika na milipuko iliyoharibu mabomba ya Nord Stream mwezi Septemba mwaka jana, madai ambayo yametupilia mbali na mataifa ya magharibi yaliyotoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa.

Lavrov alikuwa akizungumza katika hafla moja nchini India siku moja baada ya kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20.

Kwa upande wake Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amebani kuwa kumekuwa na mafanikio kidogo katika diplomasia na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW