SiasaUrusi
Urusi huenda ilihusika na hujuma za Kakhovka
18 Juni 2023Matangazo
Jarida hilo lililowanukuu mafundi na wataalamu wa milipuko liliripoti siku ya Ijumaa kwamba uchunguzi wake umebaini ushahidi uliopo unapendekeza, mlipuko huo ulitokea ndani.
Soma Zaidi:Maafisa wa Ukraine wasema athari za kupasuka kwa bwawa la Kakhova zitaendelea
Katika nyakati tofauti, timu za kimataifa za kisheria zinazowasaidia wanasheria wa Ukraine katia uchunguzi zimesema katika ripoti za awali za utafiti kwamba kuna uwezekano mkubwa kisa hicho katika eneo la Kherson kilisababishwa na milipuko iliyotegwa na Urusi.
Urusi imekuwa ikiituhumu Kyiv kwa kuhujumu bwawa hilo la kuzalisha umeme ili pamoja na mambo mengine, kuharibu chanzo muhimu cha maji katika rasi ya Crimea.