1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi imefanya mashambulio makubwa dhidi ya Ukraine

21 Januari 2025

Urusi imeishambulia Ukraine kwa droni 131 na kufyetuwa makombora manne usiku wa kuamkia leo ( 21.01.2025). Hayo ni kwa mujibu wa kikosi cha jeshi la anga cha Ukraine.

Vita vya Urusi na Ukraine
Urusi imefanya mashambulio makubwa ya droni na makombora dhidi ya UkrainePicha: Evgeniy Maloletka/AP/picture alliance

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limefanikiwa kudungua droni 72 huku nyingine 59 zikitoweka kabla ya kufikia maeneo iliyolenga kuyashambulia.

Kikosi hicho cha anga cha Ukraine kimesema, kwamba baadhi ya majengo yaliharibiwa na mashambulio hayo kwenye mikoa miwili ya Ukraine lakini  hakuna vifo vilivyotokea.

Urusi,Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha

Kwa upande mwingine jeshi la  Ukraine limesema limeshambulia miundo mbinu ya Urusi ya kiwanda cha utengenezaji  ndege kwenye eneo la Smolensk, pamoja na kituo cha mafuta katika mkoa wa Voronezh.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW