1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaanzisha wimbi la mashambulizi ya "droni", Ukraine

19 Novemba 2023

Urusi imefanya mashambulizi kadhaa ya ndege zisizokuwa na rubani alfajiri ya leo mjini Kyiv, huu ukiwa ni usiku wa pili mfululizo, inapoimarisha mashambulizi yake katika mji mkuu wa Ukraine.

Ukraine | Uhamasishaji wa wanajeshi wa Ukraine kujiunga na operesheni za kuulinda mji wa Avdiivka
Mwanajeshi wa Ukraine akiwa katika harakati za mapambano dhidi ya wanajeshi wa Urusi katika operesheni iliyolenga mahandaki ya wanajeshi wa Urusi kupitia Jimbo la Donetsk, Oktoba 20, 2023.Picha: Ozge Elif Kizil/Anadolu/picture alliance

Mkuu wa utawala wa kijeshi mjini Kyiv Serhiy Popko amesema kupitia Telegram kwamba Urusi ilianzisha wimbi la mashambulizi ya droni kutokea pande tofauti huku wakibadilisha mara kwa mara, hatua iliyosababisha kutolewa kwa tahadhari za mashambulizi ya anga mara kadhaa kwenye jiji hilo.

Jeshi la anga la Ukraine limesema mifumo yake ya kujilinda angani ilidungua droni 15 kati ya 20 zilizorushwa na Urusi kuelekea miji ya Kyiv, Poltava na Cherkasy.

Popko amesema hakuna ripoti yoyote ya uharibifu mkubwa, vifo ama watu kujeruhiwa, na kuongeza kuwa karibu droni 10 ziliangukia Kyiv na kwenye viunga vyake.    

Kyiv na Moscow zimeshambuliana usiku wa Jumamosi, ingawa pande zote mbili zimedai kuwa zilizuia mashambulizi mengi na hakuna athari iliyoripotiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW