1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege zisizo na rubani

10 Septemba 2023

Urusi imefyatua zaidi ya makombora 30 kuelekea Ukraine mapema leo Jumapili, huku kukitokea milipuko karibu na mji mkuu Kyiv pamoja na maeneo ya karibu kwa takriban saa mbili.

Russischer Drohnenangriff in Kiew
Picha: Gleb Garanich/Reuters

Jeshi la anga la Ukraine limesema limedungua ndege zisizo na rubani 26 kati ya 33 za Urusi ambazo zilikuwa zimelenga mji mkuu wa Kyiv na mikoa ya karibu.

Soma pia: Rais wa Urusi Vladmir Putin atoa wito wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja zote na Korea ya Kaskazini

Kulingana na Meya ya Kyiv Vitali Klitschko mabaki ya ndege hizo yalianguka katika wilaya tano tofauti na mtu mmoja amejeruhiwa.Hata hivyo Urusi haikutoa maoni yoyoyte kuhusu mashambulizi hayo.

Moscow imefanya mashambulizi ya anga ya mara kwa mara dhidi ya Ukraine katika maakaazi ya watu, mbali na uwanja wa vita upande wa mashariki na kusini tangu ilipoanzisha uvamizi wake miezi 18 iliyopita.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW