1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi imelifunga bomba la gesi inayoingia Ujerumani

11 Julai 2022

Urusi imelifunga bomba la Nord Stream 1 kwa kile ilichoeleza kuwa ni kulifanyia ukarabati, lakini Ujerumani imeonya kuwa hatua hiyo inaweza kuwa ya kudumu.

Deutschland | Gas Pipeline Nord Stream 1
Picha: Hannibal Hanschke/REUTERS

Hatua hiyo kimsingi itapunguza usambazaji wa gesi barani Ulaya, na baadhi ya maafisa wanaonesha hofu kwamba huuenda Urusi itarefusha muda wa ukarabati kwa lengo kuondosha hali ya utulivu barani Ulaya ingawa mpango wa utelekezaji wa hatua hiyo ulikuwepo tangu awali.

Mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa nishati wa Ujerumani, Klaus Müller amenukuliwa na shirika la habari la Uingereza la Reuters akisema kinachoweza kutokea baada ya kuhitimishwa ukrabari huo, hakuna anaweza kukizungumzia kwa sasa", Zaidi Müller anasema: "Kwa sasa tayari, bili za watumiaji wa gesi zimepanda zaidi lakini ongezeko hilo lilianza katika vipindi vya vuli na baridi vilivyopitata. Na pia bado haviakisi hali ya vita vya Ukraine na kiwango cha onyo la mapema la gesi. Kuna tishio la ongezeko kubwa la bei ambalo waagizaji wa gesi tayari wanapaswa kulipa sasa. Hiyo ni sababu mojawapo iliyofanya Uniper kuomba msaada wa serikali."

Jitihada ya kupunguza utegemezi kwa Urusi.

Kiwanda cha magari aina ya Volkswagen Picha: Jens Meyer/AP/picture alliance

Ujerumani na mataifa mengine ya Ulaya yapo katika jitihada yao ya kupunguza utegemezi wa uagizaji wa nishati  kutoka Urusi. Ujerumani kwa mfano, taifa ambalo lina uchumi mkubwa barani Ulaya ilimekuwa likitumia asilimia 35 ya gesi kwa matumizi ya kiviwanda na kuzalisha nishati ya umeme.

Mwezi uliopita makamo wa Kansela Robert Habeck alizindua awamu ya pili ya taifa lake ya jitihada ya mpango wa dharura wa hatua ya tatu katika usambazaji wa gesi asilimia, huku akionya kwamba kitovu cha uchumi wa Ulaya kinakabiliwa na janga na hasa katika hifadhi nishati yake kuelekea katika msimu wa baridi.

Mji wa Kharkiv unashambuliwa vibaya.

Ndani nchini Ukraine majeshi ya Urusi yameongeza mashambulizi yake katika mji wa pili kwa ukubwa wa taifa hilo Kharkiv, kwa lengo la kuongeza udhibiti katika miji ya mashiriki ya Ukraine.  Gavana wa eneo hilo Oleh Syneihubov kupitia ukurasa wake wa telegram amesema vikosi vya Urusi vinashambulia maeneo ya raia.

Soma zaidi:Blinken aitaka Urusi kuruhusu nafaka ya Ukraine kusafirishwa nje

Ameyataja maeneo matatu yaliovurumishiwa makombora ya Urusi kuwa ni shule, jengo la makazi na kombora la tatu lilitua karibu na eneo la ghala. Mashambulizi hayo yametokea siku mbili tu baada ya shambulio la roketi la Urusi kuvunja majengo ya ghorofa mashariki mwa Ukraine, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua watu 19.

Vyanzo: AP/RTR/DW