1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi imesema imekidhibiti kijiji karibu na Bakhmut

20 Februari 2023

Urusi imesema kwamba vikosi vyake vimechukua udhibiti wa kijiji karibu na mji wa Bakhmut, mashariki mwa Ukraine.

Ukraine-Krieg | Ukrainische Soldaten an der Front bei Bachmut
Picha: Libkos/AP Photo/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wapiganaji wa kujitolea wamekomboa eneo la makaazi ya Paraskoviivka, kwa msaada wa vikosi vya kawaida vya jeshi.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijawataja wapiganaji wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi ya Wagner Group, ambao siku ya Ijumaa walidai kukidhibiti kijiji hicho.

Kiongozi wa Wagner, Yevgev Prigozhin, amesema inaweza ikachukua miezi kadhaa kuukomboa mji wa Bakhmut, ambao umegeuka kuwa eneo muhimu la kisiasa.

Mwezi Januari, Prigozhin alidai wapiganaji wake wamechukua udhibiti karibu na Soledar. Siku mbili baadae wizara ya ulinzi ilisema vikosi vya Urusi vinaudhibiti mji huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW