Urusi yakana madai ya kuvuruga utulivu wa kikanda
3 Mei 2024Matangazo
Jana Alhamis, Wizara ya Mambo ya Nje ya taifa hilo ilisema kwamba "tuhuma dhidi ya Moscow na Pyongyang katika ushirikiano wa kijeshi hazina msingi na wala uthibitisho."
Aprili 25, Shirika la Habari la Uingereza Reuters liliripoti kwamba kumekuwa na taarifa za kichunguzi zinazoonesha meli ya mizigo ya Urusi iliyowekewa vikwazo inasafirisha silaha kutoka Korea Kaskazini kwenda Urusi.
Duru zinaonesha tangu Agosti 2023 meli hiyo imefanya safari mara 11 kati ya Bandari ya Korea Kaskazini ya Rajin na bandari za Urusi.