1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aapa kujibu vikali mashambulizi ya Ukraine

16 Machi 2024

Rais Vladimir Putin ameapa kujibu vikali msururu wa mashambulizi yaliyofanywa na Ukraine kwenye mpaka wa Urusi ambayo ameyataja kuwa ni jaribio la Kyiv la kuvuruga azma yake ya kuchaguliwa tena.

Urusi | Putin akilihutubia taifa
Rais Vladimir Putin akilihutubia taifa katika hotuba ya kila mwaka mjini Moscow. Putin ameahidi kulipiza vikali mashambulizi ya sasa ya UkrainePicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Rais Putin alisema hayo alipolihutubia baraza lake la usalama katika siku ya kwanza ya uchaguzi unaofanyika kwa siku tatu ndani ya nchi hiyo na kwenye maeneo inayoyakalia kimabavu nchini Ukraine.

Putin ameahidi kujibu vikali mashambulizi hayo ya anga ya Ukraine kwenye maeneo ya mpakani ya Belgorod na Kursk yanayokabiliwa na mapigano makali katika siku za hivi karibuni na makundi yanaiunga mkono Kyiv na kusisitiza kwamba hilo ni jaribio la kuingilia uchaguzi wa rais.

Putin amekuwa madarakani tangu mwaka 1999 na anatazamiwa kusalia madarakani hadi 2030.