1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi kujadili muswada juu ya wakosoaji wa jeshi lake

20 Januari 2024

Spika wa bunge la Urusi Vyacheslav Volodin amesema nchi hiyo inazingatia kuupitisha muswada ambao utataifisha mali na fedha za mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kusambaza "habari za uwongo" kuhusu jeshi la Urusi.

Vyacheslav Volodin
Spika wa bunge la Urusi Vyacheslav VolodinPicha: Anton Novoderezhkin/ITAR-TASS/IMAGO

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, muswada huo ambao unaungwa mkono na wabunge wote nchini humo, utawasilishwa bungeni siku ya Jumatatu ili ujadiliwe.

Moscow imefanya ukosoaji wa jeshi kuwa kosa baada ya kuivamia Ukraine mnamo mwezi Februari 2022, na imewakatama maelfu ya watu wanaopinga uvamizi huo.

Vyacheslav Volodin amesema hatua hiyo inalenga kuwaadhibu wale aliowaita "mafisadi" ambao wanalipaka tope jeshi la Urusi na maafisa wengine wanaoendelea na oparesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW