1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kulipiza kisasi jaribio la 'kumuua Putin'

5 Mei 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema shambulizi la ndege isiyo na rubani katika ikulu ya Urusi, Kremlin, kilikuwa "kitendo cha uhasama" na nchi hiyo itajibu kwa kuchukua hatua madhubuti.

Russland Vladimir Putin per Video nimmt an der Einweihung des türkischen Kernkraftwerks Akkuyu teil
Picha: SPUTNIK via REUTERS

Urusi inaishutumu Ukraine kwa kurusha ndege hiyo katika ikulu ya Kremlin katika jaribio la kumuua Rais Vladmir Putin.

Urusi imesema Marekani inahusika kupanga shambulizi hilo.

Akizungumza leo na waandishi habari nchini India, Lavrov amesema ni wazi kwamba "magaidi wa Ukraine wasingeweza kufanya hivyo peke yao bila Marekani kufahamu."

Soma zaidi: Ukraine: Putin azuru mikoa miwili inayokaliwa na Urusi

Hata hivyo, Ukraine imekanusha madai hayo na Marekani imeyapuuza ikisema ni ya "uongo".

Wakati huo huo, kiongozi wa kundi binafsi la kijeshi la Urusi, Wagner, Yevgeny Prigozhin amesema kikosi chake kitaondoka Bahkmut, Ukraine Mei 10.

Prigozhin amesema leo kuwa wataondoka kwa sababu ya kupoteza wapiganaji wake wengi na ukosefu wa silaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW