1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi kupunguza uzalishaji wa mafuta

10 Februari 2023

Urusi imesema itapunguza uzalishaji wa mafuta ghafi kwa kiwango cha asilimia tano kuanzia mwezi ujao ikiwa ni kukabliana na hatua ya mataifa ya magharibi ya kuweka ukomo wa bei.

Russland Energieminister russia Alexander Nowak
Picha: Sergei Pyatakov/ITAR-TASS/IMAGO

Naibu Waziri Mkuu wa Urusi, Alexander Novak amesema Urusi itapunguza uzalishaji wa mafuta ghafi kwa kiwango cha asilimia tano kuanzia mwezi ujao ikiwa ni kukabliana na hatua ya mataifa ya magharibi ya kuweka ukomo wa bei.

Novak amesema kuanzia Machi, Urusi itapunguza uzalishaji wa mafuta mapipa 500,000 kwa siku. Hatua hiyo amaesema inakusudia kudumisha mahusiano ya soko.

Urusi ni sehemu ya muungano na matiafa yenye kuzalisha mafuta kwa wingi dubniani OPEC ambao hukutana mara kwa mara ili kuamua viwango vya pato la mafuta.

Kutokana na operesheni ya kijeshi ya serikali ya Moscow nchini Ukraine, nchi za Magharibi zimepunguza bei, hatua ambayo inailazimisha Urusi kuweza kuuza mafuta ghafi yake kwa kiwango cha chini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW