1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi kutafakari kulipa kundi la Wagner hadhi ya kisheria

14 Julai 2023

Urusi imesema inaweza kutoa hadhi ya kisheria kwa vikundi binafsi vya kijeshi. Badiliko hilo la msimamo lilichochewa na tofauti kati yake na kundi la wapiganaji binafsi Wagner lililofanya uasi ulioshindwa mwezi Juni.

Dmitry Peskov, msemaji wa ikulu ya rais nchini Urusi.
Dmitry Peskov, msemaji wa ikulu ya rais nchini Urusi.Picha: Sergei Savostyanov/TASS/dpa/picture alliance

Utata kuhusu uhusiano kati ya makundi kama ya Wagner na taifa la Urusi umeifanya Kremlin kukana kuwatuma wapiganaji binafsi kupigana nchi za nje kwa masilahi ya Urusi.

Lakini uasi ulioshindwa wa Wagner, umesababisha Urusi kulileta kundi hilo karibu chini ya udhibiti wake, ikiwemo kuchukua zana zao nzito za kivita, na kufanya makubaliano ya kuruhusu kiongozi wao kuishi uhamishoni.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kiongozi wa mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, alikataa wapiganaji wake kuwa chini ya kamandi ya mtu mwengine. Baada ya uasiWiki tatu baadaye kundi hilo lilijaribu uasi ulioshindwa dhidi ya wakuu wa jeshi rasmi la Urusi. Kremlin ilisema Putin alikutana na kiongozi wa Wagner. Hadi sasa mustakabali wa wapiganaji wa Wagner bado haujulikani. Rais wa Belarus Lukashenko alisema Prigozhin amerejea Urusi.

Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa kundi la wapiganaji binafsi wa Wagner ambaye aliruhusiwa kuishi uhamishoni baada ya jaribio la uasi dhidi ya wakuu wa jeshi rasmi la Urusi.Picha: AP/picture alliance

Ugumu wa utambulisho wa kisheria kwa Wagner

Akijibu swali la mwandishi habari, Dmitry Peskov , msemaji wa Rais Putin amesema suala hilo litazingatiwa. Ameongeza kuwa ni hatua itakayoipa serikali ya Urusi udhibiti wa moja wa moja wa wapiganaji wote binafsi.

Peskov amesema Rais Putin alisema "utambulisho wa kisheria wa kundi kama la Wagner PMC haupo wala haujakuwepo. Hili ni suala ambalo linapaswa kutazamwa na kuzingatiwa, na kwamba suala la hadhi ya kisheria kwa kampuni kama hizo ni gumu sana".

Soma pia: Urusi yachunguza ikiwa nchi za magharibi zilihusika na uasi

Urusi yasema Prigozhin hatashitakiwa

Hayo yakijiri, rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan, amesema amekubaliana na rais Vladimir Putin kwamba makubaliano ya usafirishaji nafaka ya Ukraine kupitia Bahari Nyeusi yanapaswa kurefushwa.

Erdogan: Makubaliano ya usafirishaji nafaka ya Ukraine kurefushwa

Erdogan amewaambia waandishi habari kwamba kufuatia juhudi za Umoja wa Mataifa nan chi yake, anamatumaini makubaliano hayo yatarefushwa kutoka tarehe ya mwisho ya sasa ambayo ni Julai 17.

Urusi inaonesha hali ipo sawa baada ya uasi wa wagner

01:52

This browser does not support the video element.

Umoja wa Mataifa na Uturuki zilisaidia kupatikana kwa makubaliano hayo kati ya Urusi na Ukraine mnamo Julai mwaka 2022, kusaidia kuepusha mgogoro wa chakula ulimwenguni uliosababishwa na hatua ya Urusi kuivamia Ukraine na kuzuia bandari zake. Kulikuwa na hofu kuwa huenda Urusi isirefushe mpango wa usafirishaji nafaka.​​​​​​​

Katika tukio jingine, mahakama moja ya Ukraine imemhukumu mtu mmoja kifungo cha miaka 10 jela, baada ya kumkuta na hatia ya kupanga njama na Urusi, kulipua miundo mbinu ya usafiri ili kuhujumu usafirishwaji wa silaha ambazo nchi nyingine zinaipa Ukraine.

Hayo yamesemwa na mamlaka ya usalama wa ndani nchini Ukraine. Hata hivyo mamlaka hiyo haikuweka wazi utambulisho wa mtu huyo.

(Vyanzo: AFPE, RTRE)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW