1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi kutengeneza vifauru 1,500 kwa ajili ya vita Ukraine

23 Machi 2023

Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev amesema Urusi imepanga kutengeneza vifaru 15,000 kwa mwaka huu kwa ajili ya makabiliano yake na Ukraine.

Russland | Dmitri Medwedew
Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev.Picha: Alexei Maishev/TASS/IMAGO

Kupitia ukurasa wake wa telegram, rais huyo wa zamani wa Urusi amesema kiwanda cha kijeshi kinasonga mbele pamoja na kwamba mataifa ya Magharibi yanajaribu kuonesha taifa hilo linaishiwa mizinga, vifaru na makombora.

Hivi karibuni, Medvedev, ambaye pia anahusika na sekta ya uzaliashaji wa silaha katika Baraza la Usalama, alizungumzia juu ya kujenga na kuviboresha idadi kubwa ya vifaru wakati alitembelea kiwanda kimoja nchini humo.

Hata hivyo wataalamu wanaonesha mashaka kama Urusi inaweza kuwa na uwezo wa kuzalisha kiwango hicho cha vifaru.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW