SiasaUrusi
Urusi: Mataifa ya Magharibi yalitaka tujadiliane na Ukraine
28 Desemba 2023Matangazo
Hii ni kutokana na kile Urusi ilichokitaja kuwa Marekani na washirika wake wameshindwa kuvishinda vikosi vya Urusi nchini Ukraine.
Katika mahojiano na mashirika ya habari yenye kuegemea serikali ya Urusi, Lavrov amesema kulikuwa na ishara kwamba mataifa ya Magharibi yalikuwa yanabadili mbinu na mikakakti yake kuhusu Ukraine huku akisisitiza kuwa Moscow itafikia malengo yake nchini Ukraine.
Mara kadhaa Rais wa Urusi Vladimir Putin amerudia kusema yuko tayari kwa mazungumzo ya amani na Ukraine lakini kwa kuzingatia masharti ya Urusi.
Ukraine imesisitiza haita pumzika hadi pale itapoviondoa vikosi vya Urusi kwenye ardhi yake.
Hata hivyo mataifa ya Magharibi yanasema hayataishinikiza Kyiv kuketi kwenye meza ya mazungumzo ya amani.