1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi: Matumizi ya simu chanzo cha shambulizi la Ukraine

4 Januari 2023

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema matumizi yasiyokubalika ya simu ya mkononi ndiyo yaliyochangia shambulizi la kombora kutoka Ukraine, ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi 89.

Ukraine Donezk | Angriff auf russische Militär-Unterkunft nahe Makiiwka
Picha: ALEXANDER ERMOCHENKO/REUTERS

Wizara hiyo imesema ni dhahiri kuwa simu hiyo ilimwezesha adui kubaini mahali waliko na kushambulia eneo hilo kwa kombora, ambalo awali ilikuwa imesema limeuwa wanajeshi 63 katika Mkesha wa Mwaka Mpya.

Kauli ya wizara hiyo imejiri mnamo wakati kuna ongezeko la ghadhabu miongoni mwa wachambuzi nchini Urusi, ambao wanakosoa kile wanachosema ni uzembe uliopelekea vifo vya wanajeshi wao.

Hasira nyingi mitandaoni zilielekezwa kwa makamanda wa jeshi na si kwa Rais Vladimir Putin, ambaye hajazungumza hadharani, kuhusu shambulizi hilo, ambalo ni pigo jingine dhidi ya vikosi vyake vilivyojiondoa kwenye baadhi ya maeneo ya mapambano, katika miezi ya hivi karibuni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW