Urusi na China zazuwia azimio la UN kufungua Hormuz
8 Aprili 2026
Matangazo
Urusi na China zimepiga kura ya turufu dhidi ya azimio la Bahrain katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililolenga kulinda usafirishaji wa kibiashara katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Katika kura hiyo, wanachama 11 waliunga mkono azimio hilo, huku China na Urusi wakilipinga, na wanachama wawili wakijizuia.
Kutokana na kura hizo za turufu kutoka kwa wanachama wa kudumu, azimio hilo halikuweza kupitishwa. Waziri wa mambo ya nje wa Bahrain, Abdullatif bin Rashid Al Zayani, amesema azimio hilo limeshindwa kupita kutokana na kura hasi kutoka kwa mwanachama wa kudumu wa Baraza hilo.
Mlango Bahari wa Hormuz umefungwa na Iran baada ya Marekani na Israel kuanzisha vita dhidi ya nchi hiyo mnamo Februari 28.