Urusi na Ukraine kurefusha makubaliano ya nafaka
12 Machi 2023Matangazo
Uturuki imeonesha imani kwamba mataifa ya Ukraine na Urusi yatakubaliana katika urefushaji wa mkataba wa kusafirisha nafaka inayokwamishwa na vita kupitia Bahari Nyeusi.
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar ameliambia shirika la habari la Anadolu kwamba Urusi na Ukraine zipo katika muelekeo wa mtazamo wenye tija na kwamba wana imani hali hiyo itatoa matokeo chanya
Urusi ilizizuia bandari zote za Ukraine baada ya uvamizi wake wa Februari 24. Lakini kwa jitihada za Umoja wa Mataifa, Uturuki, Ukraine kadhalika na Urusi kulifikiwa makubaliano Julai 2022, usafirishaji wa shehena za nafaka kutoka katika bandari tatu zilizopo katika eneo la Bahari Nyeusi uliruhusiwa.
Makubaliano ya sasa yanafikia mwisho wake tarehe 18 Machi.