1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi na Ukraine mambo bado si shwari

11 Agosti 2023

Ukraine imesema vikosi vya Urusi vimerusha makombora manne ya mwendo wa kasi chapa Kinzhal kwenye mji wa Ivano-Frankivsk na kusababisha mauaji ya mvulana mmoja.

Ukraine Nach einem russischen Raketenangriff in Saporischschja
Picha: Viacheslav Ratynskyi/REUTERS

Jeshi la anga la Ukraine limesema kuwa kombora moja liliharibiwa ndani ya Kiev. Makombora mengine yaliangukia karibu na uwanja mdogo wa ndege, miundombinu ya kiraia na eneo la makaazi.

Urusi nayo imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuimarisha maeneo yake ya mapambano kwenye maeneo mawili ya makaazi karibu na mji wa Kupiansk, kaskazini mashariki mwa Kharkiv.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimeimarisha mbinu zake kwenye maeneo ya mapambano karibu na Vilshana na Pershotravneve.

Aidha, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ametangaza leo kuwa wakuu wa vituo vyote vya kuandikisha makuruta wamefutwa kazi kutokana na madai ya ufisadi.

 

 

 

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW