1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine wabadilishana tena wafungwa

17 Julai 2024

Urusi na Ukraine zimewaachilia jumla ya wanajeshi 190 waliokamatwa katika mabadilishano ya hivi punde ya wafungwa kati ya pande hizo mbili yaliyosimamiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Urusi na Ukraine wabadilishana tena wafungwa
Urusi na Ukraine wabadilishana tena wafungwaPicha: Danylo Pavlov/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na wizara ya ulinzi ya Urusi wamesema kwamba kila upande wanajeshi wao 95 wameachiliwa.

Kupitia mtandao wa Telegram Zelensky amesema wataendelea kuwarudisha raia wake nyumbani huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikichapisha kuwa mchakato wa mazungumzo, umefanikisha watumishi wake 95 kurudishwa. 

Kyiv na Moscow wabadilishana wafungwa wa kijeshi

Kamishna wa Haki za Kibinadamu wa Urusi Tatyana Moskalkova amesema ofisi yake ilikutana na mwenzake kutoka Ukraine katika hatua ya nadra ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya maafisa kutoka Moscow na Kyiv. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kwamba wanajeshi 1,348 wa Urusi wanazuiliwa mateka nchini Ukraine, na kwamba Urusi pia imewashikilia wanajeshi 6,465 wa Ukraine. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW