1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa 500 wa vita

5 Machi 2026

Urusi na Ukraine zitabadilishana jumla ya wafungwa 500 wa kivita Alhamis na Ijumaa.

Wafungwa wa vita wa Ukraine walioachiliwa na Urusi
Wafungwa wa vita wa Ukraine walioachiliwa na UrusiPicha: Telegram/Wolodymyr Selenskyj

Haya yamesemwa na mpatanishi mkuu wa Urusi Vladimir Medinskiy huku wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ikidai kuwa wafungwa 200 wa kwanza kutoka kila upande tayari wameshabadilishwa.

Medinskiy amesema ubadilishanaji huo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya pande tatu kati ya Urusi, Ukraine na Marekani mjini Geneva walipokuwa wanatafuta mwafaka wa kuvimaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.

Haya yanafanyika wakati ambapo Ujerumani imesema kuwa itaipa Ukraine kiasi cha dola milioni 230 ili kusaidia kujibu mashambulizi ya Urusi katika miundo mbinu yake ya nishati.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Johanne Wadepuhl alipokuwa akizungumza mjini Berlin amesema ufadhili huo utatumika kununua droni na kuwalinda raia.

Wadepuhl amesisitiza kuwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unasalia kuwa sera nambari moja ya usalama kwa Ujerumani licha ya kitisho kinachotokana na vita vinavyoendelea vya Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW