1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi na Ukraine zaendelea kupambana vikali

19 Agosti 2024

Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana vikali usiku wa kuamkia Jumatatu.

Uharibifu katika mji wa Kursk ndani ya Urusi
Ukraine imesema jeshi lake la anga limeharibu madaraja muhimu na ya kimkakati katika ardhi ya Urusi huko Kursk.Picha: Yan Dobronosov/AFP

Jeshi la anga la Ukraine limesema limeharibu droni zote 11 zilizorushwa na Urusi katika maeneo ya Mykolaiv, Cherkasy, Vinnytsia, Kyiv, Dnipropetrovsk, Kharkiv, Sumy na Donetsk.

Hayo yanajiri wakati jeshi la Ukraine likiendeleza operesheni yake katika ardhi ya Urusi huko Kursk ambako limesema limeharibu madaraja muhimu na ya kimkakati na hivyo kusambaratisha njia za kusambazia vifaa za jeshi la Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, amesema uvamizi wa jeshi lake katika eneo la Kursk huko Urusi unalenga kubuni eneo salama litakaloizuia Urusi kufanya mashambulizi kuvuka mpaka wa Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW