1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine zaendelea kupambana vikali

28 Septemba 2024

Urusi imesema vikosi vyake vinasonga mbele zaidi mashariki mwa Ukraine.

Mashambulizi ya Urusi katika mji wa Izmail, Ukraine
Mashambulizi ya Urusi katika mji wa Izmail, UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Moscow imesema vikosi vyake vimechukua udhibiti wa kijiji cha Marynivka katika mkoa wa Donetsk, na sasa vinaelekea kwenye mji muhimu wa Pokrovsk.

Jeshi la Ukraine halikutoa taarifa yoyote kuhusu kukamatwa kwa mji huo lakini likasisitiza kuwa mapigano makali yamekuwa yakiendelea karibu na eneo hilo na kwamba wameyazima  mashambulizi kadhaa ya Urusi  karibu na mji huo wa Pokrovsk.

Hayo yakiripotiwa, watu watatu wameuawa nchini Ukraine kufuatia shambulizi la droni la Urusi kwenye bandari ya Izmail iliyopo kwenye mto Danube, bandari ambayo ni muhimu kwa usafirishaji wa nafaka za Ukraine.