1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zakabiliana vikali

30 Agosti 2024

Urusi na Ukraine zimekabiliana vikali kivita usiku wa kuamkia Ijumaa, ambapo droni na mashambulizi ya anga yamesababisha watu 9 kujeruhiwa vibaya na mali kuharibiwa.

Vita vya Ukraine | Mashambulizi ya Urusi katika mkoa wa Sumy wa Ukraine
Jengo lililoshambuliwa na droni lililowaua watu wawili na kujeruhi 19 katika mji wa Sumy mashariki mwa Ukraine Julai 3, 2023,Picha: ERGEY BOBOK/AFP/Getty Images

Makabiliano hayo yanafanyika katika wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels kwa lengo la kujadili namna ya kutoa mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine katika makabiliano yao na Urusi.

Taarifa za ndani katika maeneo hayo zinaeleza kuwa shambulizi kubwa la anga limeharibu miundombinu ya raia katika mji wa Sumyna kusababisha mripuko wa moto. Mji huo wa Ukraine upo katika eneo la mpaka na Urusi, ambapo kwa upande wa Urusi kuna ule mji ambao kumeripotiwa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Ukraine wa Kursk.

Idadi ya watu 9 wamejeruhiwa katika mashambulizi

Kumpitia ukurasa wa telegram wa mamlaka ya kanda hiyo kumetolewa taarifa ya majeruhi, ingawa hakukuwa na taarifa za kina zaidi kuhusu hali ilivyo. Jeshi la Ukraine kadhalika limetoa taarifa ya mashambulizi ya makombora na droni 18. Taarifa hiyo inasema droni 12 ziliweza kudhibitiwa.

Chanzo kingine kutoka upande wa Urusi kimetoa taarifa ya kufanyika mashambulizi pamoja na mkoa huo wa Sumy lakini pia Kryvyi Rih, Poltava  ikiwa mji ya mkoa wa  Vinnytsia.

Mashambulizi 200 yametokea katika kipindi cha masaa 24

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa wameketi ndani ya gari baada ya kurejea kutoka eneo la Kursk la Urusi, karibu na mpaka wa Urusi na Ukraine Agosti 14, 2024.Picha: Evgeniy Maloletka/AP/picture alliance

Wakati huohuo idadi ya makabiliano imeongezeka kwa zaidi ya mara 200 katika majumuisho ya siku moja tu. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya mkuu wa majeshi ya Ukraine. Mapigano makali zaidi yaliripotiwa tena kutoka eneo la Pokrovsk katika mkoa wa mashariki wa Ukraine wa Donetsk, ambapo jeshi la Urusi limeripotiwa kusonga mbele.

Mapema usiku katika kijiji cha Karlivka kinachoshindaniwa kwa muda mrefu, vikosi vya Urusi viliweza kupandisha bendera yao. Kuna ripoti zinazokinzana kutoka eneo la Kursk zikieleza kuwa askari wa Urusi wamefanikiwa tena udhibiti wa Kijiji muhimu cha kimkakati cha Korenovo.

Hata hivyo taarifa ya wapiganaji wenye kupihana bega kwa bega na jeshi la Urusi inasema kuwa kuna jitihada ya vikosi vya Ukriane kujipanga upya hatua ambayo inaonesha mapigano katika juhudi ya kukikomboa kijiji hicho bado yanaendelea.

Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wakutana mjini Brussels

Nje ya maeneo ya vita mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kwa ajili ya kujadili operesheni inayondelea ya kuwapa mafunzo wanajeshi wa Ukraine ili waweze kulilinda taifa lao didi ya uvamizi wa Urusi. Mpango wa mafunzo hayo kutolewa ndani ya Ukraine pia utajadiliwa.

Kwa wakati huu mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine yanafanyika Ujerumani na Poland. Mpango wa mafunzo ulianza Novemba 2022. Kwa mujibu wa rekodi za Umoja wa Ulaya hadi hivi sasa wanajeshi 52,000 wamepata mafunzo. Umoja wa Ulaya unataka kutoa mafunzo kwa wanajeshi wengine 60,000 hadi ifikapo mwisho wa msimu huu wa kiangazi kwa 2024.

Soma zaidi: Urusi inajitahidi kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine Kursk

Pamoja na mjadala huo lipa suala la kuongeza mpango wa mafunzo hadi kufikia mwaka 2026. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiungwa mkono na Lithuania, wanataka mafunzo ya wanajeshi wa yafanyike ndani ya Ukraine lakini baadhi ya mataifa wanachama ya Umoja wa Ulaya ikiwemo Ujerumani zimeonesha mashaka na hatua hiyo.

Vyanzo: RTR/DPA

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW